ANGALIA, SIKILIZA NA ISHI Kitabu cha kwanza: Mungu hapo mwanzo
Outline: Adam, Noah, Job, Abraham. 24 sections. It has a picture book to go along with the recording.
Script Number: 418
Language: Swahili: Tanzania
Theme: Sin and Satan (Judgement, Sin, disobedience, Satan (the devil)); Christ (Sacrifice / Atonement); Eternal life (Salvation); Character of God (Grace and Mercy, Nature, character of God, Word of God (the Bible)); Living as a Christian (Worship, Obedience, Faith, trust, believe in Jesus); Bible timeline (Creation, Prophecy, fulfillment of, Gospel, Good News); Problems (Problems, troubles, worries)
Audience: General
Purpose: Teaching
Features: Monolog; Bible Stories; Extensive Scripture
Status: Approved
Scripts are basic guidelines for translation and recording into other languages. They should be adapted as necessary to make them understandable and relevant for each different culture and language. Some terms and concepts used may need more explanation or even be replaced or omitted completely.
Script Text
Utangulizi
Mfululizo huu wa pichi na kaseti umetolewa na Language Recordings Internaional
Tumefurahi kwamba wewe umejiunga pamoja sazi leo ili kusikiliza kaseti na kuangalia
picha. Katika kaseti hii tutajifunza kuhusu mtu wa kwanza aliye ishi duniani. Tutafunzwa
mambo mengi kuhusu Mungu. Angalia katika kitabu chako cha RED. Unaposikia sauti
hii ___________ ufungue picha inayofuata. Sasa ufungue katika picha ya kwanza kisha
tutaanza.
Picha ya kwanza: Adamu na wanyama
Mwanzo 1:1 - 2:14
Nataka kukuambia kuhusu Mungu na Roho mtakatifu ambaye aliumba vitu vyote. Hakuna mtu aliye muumba Mungu. Ni Mungu tu aliyeumba vitu vyote. Hapo zamani za kale hapakuwa na ardhi wala mti, wala mito. Hapakuwa na jua, mwezi wala nyota. Lakini Mungu alikuwepo. Mungu yupo hatakufa kamwe. Kuna Mungu mmoja tu. Kila afanyacho Mungu ni chema. Mungu hafanyi makosa. Kila anachoche sema Mungu ni kweli . Mahali napoishi Mungu ni mbinguni. Mungu aliumba jua, mwezi na nyota. Pia Mungu aliumba mbingu na nchi. Aliumba milima na bahari. Aliumba miti, majani na aina zote za chakula tunacho kula. Mungu aliumba samaki na ndege wote. Mungu aliumba wanyama wote na wadudu pia. Kisha Mungu akamuumba mtu. Mungu alichukua mavumbi ya ardhi na kutengeneza mwili wa mwanadamu. Kisha Mungu akampulizia mwanadamu pumzi ya uhai na mwanadamu akawa hai. Akamwita jina lake Adam. Pia Mungu aliumba roho na malaika. Bwana Mungu akaona kila kitu kuwa ni chema.
**MB** Rafiki yangu, Mungu aliumba vitu vyote na ana amri juu ya vitu vyote, naye ni Mungu mwenye nguvu nyingi. Mungu anawapenda watu wote wa kila mahali na anataka kuwasaidia. Kwasababu hiyo inafaa kumpa Mungu heshima, tutii maagizo yake na tumuombe atutawale sisi.
Picha ya pili: Vituvyote mwanadamu alivyohitaji
Mwanzo 2:15-25
Mungu akafanya bustani yenye rutuba nzuri(ni mahali pazuri sana) kwa ajiri ya kukaa Adam, kulikuwa na miti mizuri, matunda mazuri na chakula kizuri. Mungu akamwambia Adamu aitunze bustani pamoja na wanyama. Mungu akawaleta wanyama wote na ndege mbele ya Adam, naye Adam akawapa majina. Mungu akampa Adam mamlaka ya kutawala vitu vyote vilivyoumbwa katika nchi. Lakini hapakuwa na msaidizi wa kumfaa Adam. Mungu akasema, "Si vema mtu huyu awepeke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye". Mungu akampa Adam usingizi mzito. Kisha Mungu akatwaa ubavu kutoka kwa Adam na akamuumba mwanamke. Adam alipoamka katika usingizi Mungu akamleta mwanamke mbele ya Adam. Mwanamume na mwanamke walikuwa uchi lakini hawa kuona haya. Waliweza kuongea na Mungu kama marafiki. Mungu alipowaumba pale bustanini hawakuwa na huzuni, kifo wala hawakuwa na uovu.
Picha ya tatu: Dhambi iliingia
Mwanzo 3:1-8
Mungu akamwambia Adam na mwanamke kwamba wange weza kula matunda ya miti yote ambayo amewapa. Lakini kuna mti wa katikati, Bwana Mungu akasema "msile matunda ya mti ule wa katikati na sikumtakapo kula hikika mtakufa. Huu ni mti ambao ungeweza kumpa mtu ujuzi wa kujua mema na mabaya. Shetani alikuwa malaika mbinguni, lakini alimuasi Mungu. Shetani aliwachukia Adam na mwanamke kwasababu walikuwa marafiki wa Mungu. Kwasababu hiyo shetani akaanza kuwashawishi ili wamuasi Mungu. Shetani alitaka Adam na mwanamke wawe na uzuni, pia alitaka wafe. Siku moja shetani akamwendea mwanamke akiwa katika umbo la nyoka. Alianza kumwambia uongo. Shetani akasema hivi, "mkila matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya hamtakufa. Mtafumbuliwa macho mtakuwa kama Mungu". Mwanamke akamsikiliza nyoka, akachukua matunda akala akampa na Adam naye akala. Adam na mwanamke wote walimuasi Mungu. Walipo kula yale matunda hawakupata busara ambayo walifikiri wange pata. Badalayake waliona aibu na kujificha ili Mungu asiwaone.
Picha ya nne: Matokeo ya dhambi
Mwanzo 3:14-24
Mungu akawafukuza Adam na mwanamke watoke katika bustani. Bwana Mungu akasema Adam, "kwasababu umekula matunda niliyo kukataza, ardhi imelaaniwa kwa ajili yako. Utafanya kazi kwanguvu na jasho iliupate chakula. Mungu akamwambia mwanamke, "utazaa kwa uchungu" Mungu akamwambia nyoka, kwasababu umeyafanya haya umelaaniwa kuliko wanyama wote, kwatumbo utakwenda na utakula mavumbi ya ardhi. Nyoka akawa adui wa mwanadam. Mwanmke jina lake akaitwa Eva yaani maana yake ni mama wawote. Eva akawa na mtoto ambaye ndiye babu yetu sisi sote. Sisi bado tumetengwa na Mungu na tumemuasi kama Adam. Lakini Mungu akaahidi kwamba siku moja angemtuma mtu ambaye angemshinda shetani. Angekuwa na uwezo wa kutupeleka kwa Mungu. Mtu huyo anaitwa Bwana Yesu Kristo.
Picha ya tano: Nuhu mtu wa haki
Mwanzo 3:14-24
Sasa ni miaka mingi ukoo wa Adam umeongezeka, na watu wamekuwa wengi duniani. Lakini watu waliozaliwa na ukoo wa Adam walifanya yale yale ambayo babu zao walifanya. Walimuasi Mungu na kufanya mambo yao. Lakini alikuwepe mtu mmoja jina lake Nuhu. Nuhu alikuwa mtu aliyempenda Mungu na kumcha. Mungu akasema Nuhu ni mtu mwema ambaye ananipendeza sana. Mungu akamwambia Nuhu, "mambo yote anayo waza na kutenda mwanadamu ni uovu. Kwa hivyo nitaleta mafuriko ya maji na itawaangamiza wote, nilazima wewe Nuhu utengeneze safina. Kisha wewe na familia yako na wanyama wako mtaingia ndani ya safina na kuwa salama." Nuhu pamoja na wanawe watatu wakafanya kazi ngumu sana na kujengeneza safina kwa miaka miamoja na ishirini. Kama Mungu alivyo mwagiza. (SE) Nuhu kawaambia watu vile Mungu alivyo sema. Lakini watu walimcheka sana. (SE) Watu hawakuamini maneno ambayo Munbu alikuwa amemwambia Nuhu, na wakaendelea kufanya mambo maovu. Mungu akaleta wanyama wengi kwa Nuhu, wanyama wa kike na wa kiume na kila aina ya ndege. Nuhu akawaingiza ndani ya safina. Kisha akaweka na vyakula vyote ambavyo wangehitaji. Kisha Nuhu na mke wake na watoto na wake pamoja na wakwe zake wote wakaingia katika safina. Sasa walikuwa tayari kwa galika ya maji. Kisha Mungu akafunga mlango wa safina. (local se)
Picha ya sita: Mafuriko yakaja
Mwanzo 7:1-24
Mungu kaleta mvua kubwa sana kama alivyo sema (SE) vilevile Mungu akafanya maji yawe megi juu ya nchi. Watu na wanyama waliokuwa nje ya safina walipatwa na hofu kubwa. Mvua kubwa iliendelea kunyesha kwa siku arobaini (SE) na maji yakawa mengi kupita miti na milima. Watu wote ambao hawakuwepo ndani ya safina walizama ndani ya maji. Watu hawa hawakutii maagizo ya Mungu. hawakuamini kwamba ujumbe wa Mungu ulikuwa wa kweli. Nuhu na watu wa wafamilia yake wote walikuwa salama. Hata wanyama na ndege wote wambao walikuwa ndani ya safina walikuwa salama. Watu waliokua ndani ya safina walisikia sauti ya kubwa ya mvua na waliona mafuriko juu ya nchi yote, lakini hawakudhurika kw mafuriko hayo. Kwasababu walitii maagizo ya Mungu.
**MB** Rafiki mpendwa, hivyo ndivyo ilivyo kunapo mwendea Yesu. Mungu amesema wato wote wamefanya dhambi na wote wata adhibiwa kutoka na dhambi zao. Lakini Mungu alimtuma mwanawe Yesu Kristo kutuokoa. Yesu alichukua adhabu ya dhambi zetu, alipokufa pale msalabani. Tukigeuka kutoka dhambini na kumuomba Yesu atusamehe, Bwana Yesu atatusamehe. Yesu ni kama safina ambayo Nuhu na familia yake waliingia. Tunapomwendea Yesu kunakuwa salama na atuta hukumiwa kwaajili ya dhambi zetu.
Picha ya saba: Upinde wa Mvua ni ahadi ya Mungu
Mwanzo 8:13 - 9:17
Nuhu na familia yake pamoja na wanyama wote walikaa ndani ya safina kwa muda wa mwaka mmoja. Baada ya muda maji yalianza kupungua na kukauka. Kisha watu walianza kutoka ndani ya safina, na alitembea juu ya ardhi ambayo ni kavu. Mungu aliwalinda Nuhu na familia yake. Nuhu alimshurukuru Mungu sana Mungu. kwahivyo Nuhu alichinja baadhi ya wanyama na ndege na akamtolea Mungu kama sadaka. Nuhu akatengeza madhabahu, akawaweka wanya na ndege juu ya madhabahu na kuwateketeza kwa moto. Mungu akapendezwa sana na sadaka ya Nuhu. Mungu akamwambia Nuhu na familia yake, "Ninaweka agano kwako na kwaziza chako kwamba, sinta iangamiza tena dunia kwa maji ya galika". Na ikawa kama kawaida katika dunia, wakaanza kupanda na kuvuna mazao, kukawa na kipindi cha baridi na joto, masika na kiangazi, na kukawa na usiku na mchana. Mambo hayo yaliendelea kama kawaida. Mungu akamwambia Nuhu kwamba, nitaweka upinde wa mvua juu ya mawingu, na kila wakati nitakapo uona upinde wa mvua nitakumbuka ahadi niliyo waahidi . Mungu alitaka wazaane na waijaze nchi. Nuhu na familia yake walifanya hivyo. Sisi sote tumetokana na kizazi cha Nuhu.
**MB** Rafiki mpendwa tunapofikiri juu ya habari hizi inatusaidia tuelewe kwamba maneno ya Mungu na ahadi zake ni zakweli. Ikiwa Mungu anasema atawaahukumu wenye dhambi, atafanya hivyo kama livyo fanya wakati wakizazi cha Nuhu. Ikiwa Mungu anasema atawaokoa wale wanaompenda na kumtii, yeye atafanya hivyo. Tunapo ona upinde wa mvua katika mawingu tunakumbuka kwamba maneno ya Mungu ni kweli. Kumbuka kumpenda Mungu kumtii kwa njia hiyo tutampendeza Mungu kama alivyo fanya Nuhu.
Picha ya nane: Kizazi cha Nuhu
Mwanzo 11:1-9
Baada ya galika ya maji kizazi cha Nuhu kikaongezeka kukawa na watu wengi sana katika nchi. Watu hawa wakajikusanya pamoja na kuishi. Watu hawa hawakufikiri kuhusu Mungu. Wao limsahau Mungu. Walijifikilia wao wenyewe tu. Waliamua wajenge mnala mrefu ili wajipatie jina. Walifanya kazi kubwa yakutengeneza mnala. Walifanya hivyo ilikumuasi Mungu na kujaribu kujipatia jina. Kwahiyo walijenga mnala. Lakini Mungu alijua yote waliyo fikiri na kuyafanya. Mungu akachafua lugha zao ili wasielewane. Hii ilifanya kazi ya kujenga mnala iwe ngumu. Kwasababu hiyo watu walianza kujigawa kutokana na lugha zao. Kisha wakaenda kuishi pamoja. Mungu akawamekomesha kazi ya kujenga mnala. Mungu akaharibu mpango wao na akaondoa kiburi chao. Na mahali pale pakaitwa "Babeli" maanya yake ni machafuko, kwasababu Mungu alichafua lugha za wanadam na kufanya watawanyike na kuishi sehemu mbali mbali za nchi.
**NB** Rafiki mpendwa, habari hii inatusaidia tuelewe kwamba Mungu anajua kila kitu kuhusu sisi. Kama Mungu alivyo wajua watu wa Babeli na yale waliyo kuwayafanya , basi Mungu anajua sisi na yale tunayo yafanya. Pia habari hii intufundiswa kamba Mungu ni mtawala wavitu vyote. Mungu anaweza kubadilisha maamuzi aliyofanywa na wanadam. Kwa wale wasio mtii Mungu. Mungu anaweza kubadili mambo yao iliwasi muasi.
Picha ya tisa: Ayubu mtu mkamilifu
Ayubu 1:1-12
Miaka mingi iliyopita palikuwa na mtu mmoja jina lake alikuwa akiitwa Ayubu. Ayubu alikuwa mzuri ambae alimpenda Mungu. Alijaribu kumpendeza Mungu kwa kilakila alicho fanya. Hatuka kufanya mambo maovu. Mungu alimpa Ayubu vitu vingi na vizuri. Ayubu alikuwa na famila kubwa na mwenye mali nyingi. Alikuwa mtu maarufu na tajiri sana katika nchi ile. Kila waki Ayubu aliuwa kaiwaombea watoto wake na kutoa sadaka kwa Mungu kwa niaba ya watoto wake, kama unavyo oona katika picha. Siku moja Mungu akakutana na malaika uko mbinguni shetani pia alikuwepo. Mungu akamuuliza shetani, "je umemuona mtumishi wangu Ayubu mtu mkamilifu na uaminifu?". Shetani akasema Ayubu anamcha Mungu na kumpenda kwasababu ya vitu vingi ambavyo Mungu amempa. Shetani akasema ikiwa mali zote alizonazo zikiharibiwa, Ayubu hatamcha Mungu wala hatampenda Mungu. Kwa hivyo Mungu akampa shetani ruhusa ya kumjaribu Ayubu, lakini Mungu hakutaka shetani amuue Ayube.
**MB**Rafiki mpendwa, Mungu anajua mambo yote kuhusu sisi. Mungu ufurahi anapoona mambo ambayo tunayafanya yanampendeza. Lakini hatuji mambo ambayo Mungu ametupangia katika maisha yetu. Pengine tuna weza kupata mateso sawa sawa na wale wasio mpenda Mungu. Yeye natupenda, pia anatawala vitu vyote. Mungu anatumia majaribu na mateso ilikutuimarisha sisi ili sisi tuwasaidie watu wengine.
Picha ya kumi: Wakati wa mateso makubwa
Ayubu 1:13-22
Mungu alimruhusu shetani kumjaribu Ayubu. Shetani alitaka kumjaribu Ayubu iliajue kama kweli anapenda Mungu. Shetani alimjaribu Ayubu kwa kuangamiza vitu vyake vyote. Hii ndivyo livyo kuwa. (Second Voice) Siku moja Ayubu alikuwa amekaa nyumbani kwake, mtuishi wake akaja mbio kwa Ayubu na kumwambia
"Hao ng'ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha karibu nao; mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari."
Huyo alipokuwa bado akiongea na Ayubu. Mtumishi mwingine akaja na kusema. (Third Voice) "Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari."
Huyo alipokuwa bado akiongea na Ayubu. Mtumishi mwingine akaja na kusema. (Fourth Voice) "Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari."
Huyo alipokuwa bado akiongea na Ayubu. Mtumishi mwingine akaja na kusema. (Fifth Voice) "Wanao na binti zako walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa; mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari."
(First Voice) Ayubu alipoteza malizake zote, pia alipoteza watoto wake wote kwa wati mmoja. Ayubu alikuwa na uzuni sana. Lakini hakumkufuru Mungu. Ayubu aliendelea kumpenda Mungu na kumwabudu. Ayubu akasema, "kasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe."
**MB** Rafiki mpendwa, tunapo teseka, au marafiki zetu wanapo teseka, Mungu anajua hayo yote. Mungu anajua nikwajinsi gani tunavyo umia. Yesu Christo (mwana wa Mungu) hakuwa na dhambi, lakini aliteseka. Yesu alijaribiwa kama sisi tunvyo jaribiwa. Yesu anajua mateso hayo naye anaweza kutusaidia. Yesu aliteseka mpaka kufa msalabani na kulipa deni yetu ya dhambi, lakini alifufuka baada ya siku tatu na kutupa sisi tumaini la uzima wa milele.
Picha ya kumi na moja: Mateso ya Ayubu
Ayubu 2:1 - 41:34
Tena kulikuwa na mkutano mwingine uko mbinguni na shetani alikuwepo. BWANA akamwuliza Shetani, "Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu." Shetani akajibu anakusema, Ayubu atamkufuru Mungu ikiwa atapata mateso katika mwili wake, kwani vyote alivyo navyo mtu atatoa kwa ajiri ya uhai wake. Mungu akamruhusu shetani ili amjaribu Ayubu. Lakini hakumruhusu shetani amuue Ayubu. Basi Shetani akatoka mbele za Mungu na kwenda kumjaribu Ayubu. Shetani akampiga shetani kwa majipu mwili mzima. Mateso haya yalimuumiza sana Ayubu. Ayubu akachukua kigae na kuanza kujikuna. Mke wa Ayubu alichukizwa sana na yale mateso ya Ayubu. Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu, ukafe. Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake. Basi ikawa hao rafikize Ayubu watatu walipopata habari ya mabaya hayo yote aliyo mpata, wakaja kila mtu kutoka mahali pake; nao ni Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi; wakapatana pamoja ili waende kumlilia Ayubu na kumtuliza moyo. Basi walipoangaza macho yao, nao wakali mbali, wasimtambue, wakainua sauti zao na kulia; kila mmoja akararua guo yake, wakarusha mavumbi juu ya vichwa vyao kuelekea mbinguni. Kisha wakaketi nchi pamoja naye muda wa siku saba, mchana na usiku, wala hapana mmoja aliyenena naye neno lo lote; kwa maana waliona ya kuwa mashaka yake aliyo nayo ni makuu mno. Kisha waliongea na Ayubu kwa siku nyingi. Walitaka kuelewa kwanini mateso hayo yalimpata Ayubu. Nawalisema kuteseka kwa Ayubu kunatokana na mambaya aliyo yatenda. Kama angeungama dhambi mambo hayo yasinge mpata. Ayubu alijua kwamba mambo waliyo yasema rafiki zake haya kuwa ya kweli. Ayubu hakufanya uovu wowote. Ayubu kamlilia Mungu na kumuuliza ni kwanini mateso hayo limpata? Na hakufanya jambo lolote baya mbele za Mungu.
**MB** Rafiki Mpendwa, Je, Unapata mateso sawa na yale mabayo Ayubu alipata? Je, unapata mateso kiasi kwamba watu hawaelewi juu ya mteso yako? Je, unafikiri kwamba Mungu amekusahau? Ni vizuri tuelewe kamba Mungu hawezi kutusahau sisi, anatupenda sana. Mungu anafurahi sana napoona sisi tunashinda mateso.
Picha ya kumi na Mbili: Kupona kwa Ayubu
Ayubu 42:1-17
Mungu alijua mambo yote ambayo rafiki zake Ayubu walikuwa wakiongea juu yake. Mungu akabariki Ayubu kwa mali nyingi. Mungu akufura hiswa na rafiki za Ayubu na maneno ambayo walikuwa wakiongea juu ya Ayubu. Mungu akawaambai wale marafiki wa Ayubu walete sana kwa Ayubu na wamwombe Ayubu awaombee. Kama wakifanya hivyo watakubaliwa na Mungu. Wale rafiki wa Ayubu wakaleta sadaka zao kwa Mungu na Ayubu akawaombea. Ayubu akabarikiwa sana na Mungu. Akawa na mali nyingi sana. Ndugu na marafiki wa Ayubu waja kumuona na wakampa zawadi nyingi sana. Baada Ayubu akawa na mali nyingi kulizo zile alizokuwanazo mwanzo. Pia alikuwa na watoto wakiume saba na wakike. Ayubu aliendelea kumpenda Mungu na kumtii katika maisha yake yote. Ayubu alikuwa na furaha sana.
**MB** Rafiki Mpendwa, Habari hizi za Ayubu ni za muhimu sana kwetu. Mara kwa mara tunakuwa kama Ayub. Mambo kama hayo yana weza kutokea na tukashindwa kuelewa ni kwanini yametupata. Tunapokuwa katika majaribu tunakuwa na uzuni. Mambo yote yatakayo tupata tujue kwamba tunamtegemea Mungu. Mungu ni mkubwa na anatawala juu ya vyote. Anaweza kutulinda na kutujali. Nakila kitu Mungu anachofanya kwetu nafanya kwa upendo.
Picha ya kumi na tatu: Abramu alimtii Mungu
Mwanzo 12:1 - 13:4
Palikuwa na mtu mmoja jina lake aliitwa Abramu. Abramu alimpenda Mungu na kumtii. Siku moja Mungu akamwambia Abramu, Abramu utoke katika nchi hii na uende katika nchi ambayo nitakuonyesha. Pia Mungu akampa Abramu ahadi akisema, "Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa kubwa, na wafalme watatoka kwako. Utakuwa baraka na kila taifa litabalikiwa kupiti wewe. Mungu alitaka Abramu na kizazi chake wawe ni watu wanaompenda Mungu na kumtii. Abramu akamwamini Mungu, akatoka katika nchi yake akaenda katika nchi ambayo aliambiwa atamwonyesha. Walisafi kwa siku nyingi kisha kwafika katika nchi ya Kanaani. Kisha Mungu akamwambia Abramu, hii ndiyo nchi nitakayo kupa wewe pamoja na uzao wako. Abramu kajenga madhabahu na kumtolea Mungu sadaka ya kuteketezwa. Abramu alimtukuza Mungu na kumwabudu kwa nchia hii.
**MB** Rafiki Mpendwa, Kumfuata Mungu si rahisi kila wakati. Lakini Mungu anata sisi tumtii katika kila kitu tunachofanya, kama vile Abramu alivyo mtii. Mungu ametuahidi kuwa pamoja nasi na kutubariki.
Picha ya kumi na nne: Uchaguzi mmbaya
Mwanzo 13:5-18
Abramu na mke wake Sarai, na Lutu nduguye Abramu, wote walienda katika nchi ya Kanaani. Abramu na Lutu walikua matajiri. Walikua na ngamia na punda wengi sana. Baada ya muda waliona hakuna nafasi ya kutosha kwaajiri ya wanyama wao. Na wachunga kondoo wa Abramu na wachunga kondoo wa Lutu waligombana mara kwa mara. Kwasababu sahemu ya chungia wanyama ilikuwa ndogo. Abramu aliona nivema ongee na Lutu juu ya jambo hilo. Abramu akamwambia Lutu, "Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati ya mimi na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu ndugu. Kwasababu hakuna nafasi kwasisi kuishi pamoja, uchague niwapi ungependa kuishi? Basi uchage, ukienda upande wa kushoto, nitakwenda upande wa kuli; ukienda upande wa kuli, nitakwenda upande wa kushoto. Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla BWANA hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya BWANA, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari. Basi Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki; wakatengana wao kwa wao. Abramu akakaa katika nchi ya Kanaani, na Lutu akakaa katika miji ya lile Bonde; akajongeza hema yake mpaka Sodoma. Mungu alimpa Abramu ahadi ya kwamba nchi ya Kanaani itakuwa ni nchi ya Abramu na uzao wake. Abramu aliamini Mungu atafanya hivyo. Abramu hakujichagulia mahali pakwenda, lakini alimsubiri Mungu amuonyeshe.
**MB** Rafiki Mpendwa, Mungu anajari maitaji yetu na hii ni ahadi yake. Wakati mwingina tuwaangalia watu wengine na kufikiri kwamba vitu walivyo navyo ni vuzuri kuliko vile tulivyo navyo sisi. Tujue kwamba kama tukimpenda Mungu na kumtii , Yeye ataishi katikati yetu na kutupa maitaji yetu. Mungu ameahidi kutupa baraka. NaYeye naweza kutuongezea kama apendavyo.
Picha ya kumi na tano: Abramu amsaidia Lutu
Mwanzo 14:1-24
Lutu na familia yake wali katika sehemu za mji wa Sodoma. Watu wa mti ule waliukuwa watu wabaya. Mfalme wa Sodoma, akapigana vita na wafalme wengine. Na Maadui wakaingia katia mji wa Sodoma na kuteka mateka. Wakachukua mali zote za Sodoma na vyakula vyao vyote, akaenda zao. akamtwaa Lutu, mwana wa nduguye Abramu, aliyekaa huko Sodoma, na mali yake, wakaenda zao. Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu. Abramu aliposikia ya kwamba nduguye ametekwa mateka, akawapa silaha vijana wake, waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane, akawafuata mpaka Dani. Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Dameski. Naye akarudisha mali zote, akamrudisha na Lutu nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu. Abramu aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme. Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote. Mfalme wa Sodoma akataka kumpa Abramu zawadi lakini Abramu hakukubali kwani alisema atapokea kutu chocho kutoka mkononi mwamfalme wa Sodoma. **BM** Rafiki Mpendwa, Lutu alikaa katika mti wa Sodoma, katika ya watu wabaya na familia yake lipatwa na matatizo mbali mbali. Neno la Mungu linatuambia kwamba tujitenga na uozu. Tipende kuishi na kukutana na watu wanompenda Yesu na kufanya mapenzi yake.
Picha ya Kumi na sita: Mungu alimpa Abramu ahadi
Mwanzo 15:1-21
Abramu alimsaidia Lutu pamoja na watu wafamilia yake. Lakini Abramu hakuwa nafuraha. Abramu na mkewe Sara walikuwa wazee sana na awakuwa na watoto. Abramu alianza kufikiri kwamba labda mtu mmoja katika watumishi wake angekuwa mrithi wa mali zake baada ya yeye kufa. Siku moja usiku Mungu akamwambia Abramu, Abramu usiangaike sana mimi ni Mungu wako, mimi nina kupenda. Mimi ndimi Mungu ninaye tawala na kuwapa watu mali na vitu vyote, na wewe ni rafiki yangu wakaribu sana. Abramu akajibu, Ndiyo Mungu, wewe ni Mungu mwenye nguvu, wewe ndiye uliye nipavitu vitu hivi na utajili huu, lakini bado sina mtoto ambaye atarithi mali hivi baada ya mimi kufa, na nitakapo kufa mali hizi zote zitakuwa za watumishi. Mungu akamjibu, La, watumishi wako hawata miliki mali yako. Utapata mtoto ambaye atamiliki mali yako. Mungu akamtoa Abramu nje na akamwonyesha nyote za angani, Mungu akamwambia unaweza kuzihesabu nyota hizi? Basi uzao wako utakua kama nyota kiasi kwamba utaweza kuhesabu. Abramu aliamini aliyo ambiwa na Mungu, alijua Mungu atafanya hivyo. Kwababu Abramu alimwamini Mungu, aliitwa rafiki wa Mungu. Abramu akamtolea Mungu sadaka na Mungu akamwahidi Abramu kwamba aliyo yasema atayafanya.
**BM** Rafiki Mpendwa, Mungu wetu ni yule yule wala habadiliki. Yey ni Mungu mwenye nguvu na Mungu anayetawala na kuwapa watu utajili. Mungu ametuahidi mambo mengi katika Neno lake. Mungu anataka sisi tumwamini na kumtii kama alivyo fanya Abramu, ndipo antapo mpendezwa nasi. Naye atatimiza ahadi zake kwetu.
Picha ya kumi na saba: Kuzaliwa kwa Ishmaeli
Mwanzo 16:1-16
Abramu na Sara hawakuwa na mtoto, na kwasababu hiyo Sara alikuwa na uzuni sana. Alijua kwamba Abramu anataka kuwa na mtoto. Sara kamwambia Abramu, Mungu hajatupatia mtoto, kwahivyo nitakupa msichana wangu wa kazi ili awe mke wako wa pili, msichana huyo aliitwa Hajiri. Nawe utalala naye kaipata mimba na kuzaa mtoto mtoto huyo atakuwa mtoto wangu. Na kwanjia hii tutapata mtoto. Na kwasiku hizo ilikuwa ni kitu cha kawaida kuwa na wake wawili. Abramu kafanya kama vile Sara alivyo mshauli. Sara akampa Abramu msichana wake wa kazi ili awe mkewake wa pili. Abramu akalala na huyo msichana naye akapata mimba. Hajiri alipokuwa ni mjamzito alimkuwa ni mwenye majivuno na alimdharau Sara. Sara alipatwa na uzuni sana juu ya jambo liyo. Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani wako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake". Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake. Malaika wa BWANA akamwambia, Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake. Na utamzaa mtoto, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, naye atakuwa taifa kubwa. Kwahivyo Hajiri akarudi kuishi na Sara na wakati wa kuzaa ulipofika alimzaa mtoto akamwita jina lake Ishmaeli. Baada ya miaka mingi kupita Abramu akawatoa Hajiri na Ishmaeli ili wakaishi nchi nyingine. Ishmaeli akawa baba wa Waarabu.
**MB** Rafiki mpendwa, katika habari hii tunaona kwamba Sara akufanya umauzi wa busala yaani kumpa Abramu mke wa pili, eti kwasababu Mungu hakuwapa mtoto. Sara alitaka kumlazimisha Mungu kutimiza mapenzi kwa njia nyingine ya haraka. Lakini uamuzi wake ulimletea huzuni. Inatupasa tumtumainie Mungu na kumtii. Tumsubili Mungu afanye kazi yake na kupanga mipango yake kwetu kama apendavyo.
Picha ya kumi na nane: Abramu ahadidiwa na Mungu
Mwanzo 18:1-15
Mungu alibadirisha jina la Abramu kuwa Ibrahimu, and kumpa ahadi yakwamba engekuwa baba taifa kubwa. Sarai jina lake lika Sara. Abramu alifiki kwamba Mungu angetimiza ahadi zake tumpitia Ishmaeli. Lakini Mungu akasema, "hapana". Mungu akasema kwamba Ibrahimu na Sara watapata mtoto. Ibrahimu alimpenda Mungu na alijua kwamba Mungu anauweza wote. Lakini Ibrahimu alikuwa mzee sana, na Sara likuwa mzee pia. Ibrahimu alifiki kwamba itakuwa vingumu sana kwa wao kupata mtoto, kwani wamesha zeeka. Mungu alitaka kumhakikishia Ibrahimu kwamba Yeye atatimiza ahadi yake. Siku moja Mungu akatuma wanaume watatu kwa Ibrahimu, wakiwa na ujumbe kwa Ibrahimu. Na hivi ndivyo ilivyo kuwa: Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako. Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu. Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema. Wale wageni Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani. Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara alipo sikia hayo akacheka moyoni kani alisema amekuwa mzee, hataweza kupata mtoto. BWANA akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee? Hakuna kitu ninacho mshinda Mungu. Kwa mwaka ujao nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume. Ibrahimu na Sara walishanga, kwani Mungu alituamia wale wanaume kuongea nao. Ibrahimu na Sara walijua kwamba Mungu anawajali.
**MB** Rafiki mpendwa, Mungu anajurali sisi sote. Mungu ametuahidi mambo mengi, naye atafanya kamba alivyo ahidi.
Picha ya kumi na tisa: Ibrahimu aliwahurumia watu Sodoma
Mwanzo 18:16 - 19:29
Wale wageni waliompa Ibrahimu ujumbe wa Mungu walikuwa wanaondoka kuelekea sodoma. Mungu akamwambia Ibrahimu kwamba ataenda sodoma kuona kama watu walikuwa wakifanya uovu. Jambo hili ilimfanya Ibrahimu awahurumie watu wa sodoma kwani alijua kwamba alitenda maovu mengi, na pengine Mungu ange waangamiza wote. Lakini Ibrahimu alimkubuka ndugu yake Lutu. Ibrahimu alijua kwamba Lutu alikuwa katiishi katika ya watu waovu, Lutu mwenyewe akuwa mtu mwovu. Kwahivyo Ibrahimu alianza kumuuliza Mungu juu ya watu wa sodoma. Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo? BWANA akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao. Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano. Ibrahimu akaendelea kumuuliza Mungu. Je, wakaonekana huko kumi? Je, utauharibu mji? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi. Bsi BWANA alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pakae. Ibrahimu akatoka asubuhi kwenda mahali aliposimama mbele za BWANA, naye akatazama upande wa Sodoma na Gomora na nchi yote ya hilo Bonde, akaona, na tazama, moshi wa nchi ukapanda, kama moshi wa tanuru. Lakini Mungu alimkumbuka Lutu. Mungu aliwatuma wale wanaume watatu na kupeleka ujumbe kwa Lutu kabla ya kuuteketeza mji wa sodoma.
**MB** Rafiki Mpendwa, Mungu alisikia maombi ya Ibrahimu na vile alivyo waombea watu wa Sodoma. Mungu anataka sisi tuwaombe watu wengeine. Mungu anataka watu wote wawe watoto wake. Anataka sisi tuwaombe watu wengine ili waje kwake, atakama ni watu waovu Mungu atawasamehe.
Picha ya ishirini: Mungu alimjaribu Ibrahimu
Mwanzo 21:1 - 22:19
Sara kapata mtoto, kama Mungu alivyo ahidi. Hii ilikuwa ni kwauwezo wa Mungu tu, kwasababu Ibrahimu na Sara walikuwa wazee sana. Na jina la mtoto wao aliitwa Isaka. Isaka alikuwa kijana aliye mpenda Mungu na kuwatii wazazi wake. Mungu alitaka kujua kama Ibrahimu anampenda, na kumtii. Siku moja Mungu akamwambia Ibrahimu, Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia. Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu. Ibrahimu akawaambia vijana wake, Kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, tukaabudu, na kuwarudia tena. Basi Ibrahimu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja. Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa? Ibrahimu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili pamoja. Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni. Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe. Ndipo malaika wa BWANA akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee. Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire,*fd* maana yake ni BWANA atapata.
**MB** Rafiki Mpendwa, Mungu alifurahiswa sana na Ibrahimu. Ibrahimu alimuamini Mungu na kumtii, ingawa ilikuwa nivigumu. Sisi pia tunaweza kumwamini Mungu. Nakitu cha muhimu kwetu ni kumtii Mungu kwa yale anayo taka sisi tufanye.
Picha ya ishirini na moja: Mke wa Isaka
Mwanzo 24:1 - 25:26
Isaka lipofikisha miaka arobaini. Ibrahimu aliona nivyema ampatie Isaka mke. Ibrahimu akamwita mtumishi wake aliye kuwa mzee na mwaminifu na kumbwambia. Uniahidi kwamba hutamuonza mwangu wanawake wasio mjua Mungu. Nataka wewe uende pamoja na Isaka katika nchi niliyo toka mimi. Na ukamtwalie mwangu Isaka mke na kuja naye hapa. Kisha huyo mtumishi akatwaa ngamia kumi katika ngamia za bwana wake akaenda zake, maana mali zote za bwana wake zilikuwa mkononi mwake, akaondoka, akaja mpaka Mesopotamia, mpaka mji wa Nahori. Lakini mtumishi yule hakujua nijinsi gani angeweza kumpatia Isaka mke, hivyo aliamua kumuomba Mungu. Naye akasema, Ee BWANA, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, nakuomba mambo yangu uyajalie yawe heri leo, ukamfadhili bwana wangu Ibrahimu. Tazama! Nimesimama karibu na kisima cha maji, na binti za watu wa mjini wanatoka kuteka maji, basi na iwe hivi; yule msichana nitakayemwambia, Tua mtungi wako, nakuomba, ninywe; naye akasema, Unywe, nami nitawanywesha na ngamia zako pia; basi huyu na awe ndiye uliyemchagulia mtumishi wako Isaka; na kwa hayo nitajua ya kuwa uliyemchagulia bwana wangu. Mtumishi wa Ibrahimu alipokuwa kaiendelea kuomba mshicha mzuri aliyekuwa akiitwa Rebeka akaja kuchota maji. Na yule mtumishi akamuomba Rebeka maji ya kunywa, Naye akasema, Unywe, bwana wangu, akafanya haraka, akatua mtungi wake mkononi mwake, akamnywesha. Hata alipokwisha kumnywesha akasema, Na ngamia zako nitawatekea, hata watakapokwisha kunywa. Akafanya haraka, akamwaga maji ya mtungi wake katika birika, akapiga mbio kisimani ateke, akawatekea ngamia zake wote. Basi ngamia walipo maliza kunywa Rebeka akamwambia yule mtumishi kwamba yeye ni mtoto wa Bethueli mwana wa Milka, mkewe Nahori ndungu yake Ibrahimu. Mtumishi wa Ibrahimu alifurahi sana kwasababu alijua kwamba, yule msichana ndiye aliye chaguliwa na Mungu.
**MB** Rafiki mpendwa, Mungu anajua mambo yote kusu sisi. Mungu anajua jinsi tunavyo sumbuka kupata mke au mume. Kama tukimpenda Mungu na kumtii yeye atatuonyesha mke au mume ambaye atatufaa. Mungu anajua kitugani ni kizuri kwetu, tuche Mungu atuongoze.
Picha ya ishirini na mbili: Ahadi za Mungu
Mathayo 1:18-25; Gal. 4:4-5
Rafiki mpendwa, Neno la Mungu ni kweli. Katika habari hizi tumejifunza habari za watu wenge katika biblea. Tumejifunza jinsi Mungu alivyo mwambia Adamu kwamba angemtuma mtu ambaye ange mshinda shetani. Tumijifunza habari za Nuhu na watu walivyo chagua kutenda maovu. Pia tumejifunza mfano wa Ayubu. Pia tumejifunza tutoka kwa Ibrahimu, vile Mungu anavyo timiza ahadi zake. Katika picha hii unaweza kuona picha ya mtoto ambaye anaitwa Yesu. Katika muda uliyo pangwa Yesu alizaliwa, katika nchi ya Israeli. Najina la mama yake laiitwa Mariamu, lakini baba yake alikuwa Mungu. Yesu peeke ndiye aliyo leta baraka kwa watu wote. Yeye ndiye aliye kuja kumshinda Shetani na kuturudisha sisi kwa Mungu.
Picha ya ishirini na tatu: Yesu alikuwa kwa ajiri yetu
Wagalatia 3:13-14; Mwanzo 3:15; 22:7-8 Yohana 1:29; 1Petro 1:19-20
Mungu aliwahidi watu wa Israeli kwamba siku moja atamtuma mwokozi. Wana wa Israeli walimsubiri mokozi kwa miaka mingi. Na Yesu alipokuja wana wa Israeli hawakufikiri kwamba angeteseka na kufa. Na miaka mingi kabla ya kuja Yesu, Mungu alitumia wajumbe wake na kutabili kwamba Mwokozi angakuja duniani na kufa kwa ajili ya dhambi za watu wote. Yohana mbatizaji alipomuona Yesu alisema, "Mwana kondoo wa Mungu aichukuye dhambi ya ulimwengu", Yesu aliteseta na kufa ili azichukue dhambi za ulimwengu wote. Nabii Isaya aliandika aliandika katika kitabu cha akisema, Mwokozi atakuja na kuteswa, kudhihakiwa, kudharauliwa na kuadhibiwa kwa ajili ya dhambi zetu, ili sisi tupate onoleo la dhambi.
**MB** Rafiki mpendwa, Mungu anasema katika neno lake kwamba watu wote wamefanya dhambi. Na adhabu ya dhambi ni kifo. Hakuna njia yeyote ambayo tunaweza kukwepa adhamu hii. Lakini Mungu alitupenda Mungu hapendi sisi tupate adhabu hii ndiyo maana akamtuma mwana wake wa Yesu Kristo kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Yesu aliteseka na kufa ili kubeba adhabu ya dhambi zetu. Sasa tukienda mbele za Yesu na kumuomba msamaha wa dhambi zetu, Yeye atatusamehe. Inatupasa mtumshukuru Mungu kwa kumtuma Yesu afemsalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Tukimwamini Yesu na kumpenda, tutaweza kutii neno lake.
Picha ya ishirini na nne: Ishi kwa kuokolewa
Ayubu 19:25-26; Isaya 53:19-29; 1wakolitho 15:3-4; Waebrania 11:19
Yesu alikuwa masalabani ilikulipa deni yatu ya dhambi. Rafiki wa Yesu wali ubeba mwili wa Yesu kutoka msalabani alipokuwa amekufa na kwenda kuzikwa. Siku ya tatu Yesu alifufuka kutoka kaburini. Yesu ni mwana wa Mungu na kifo hakiwezi kumshinda. Yesu alipofufuka kutoka katika watu aliwatokea wanafunzi wake. Wanafunzi walishangaa sana kwani hawakudhani kwamba mambo yao yangeweza kutokea. Mwanafunzi mmoja aliyeitwa Tomaso, akumuona Yesu laipo watokea wanafunzi wake. Hivyo Tomaso akuamini kwamba Yesu amefufuka. Tomaso alisema lazima amuone Yesu na kumgusa sehemu za mwili wake ndipo atakapo amini. Baadaye Yesu akamtokea Tomaso na wanafunzi wengine. Na Tomaso akaamini kwamba amafufuka. Yesu akamwambia Tomaso, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wana heri wale wasioona, wakaamani. Wanafunzi wa Yesu hawakuwa watu wa kwanza kuamini kwamba Mungu atamfufua Yesu. Fikiri kuhusu Ibrahimu alipoenda kumtoa Isaka kama sadaka. Ibrahimu alimwamini Mungu kwamba angefanya muujiza. Pia tukifikira kuhusu Ayubu alipojaribiwa kwa mateso makubwa. Ayubu aliamini kwamba Mungu atafanya miujiza. Nabii Isaya alipotabili juu ya Yesu alisema. Mwokozi atakuja duniani, kuteseka na kufa na atafufuka tena. Katika habari ya Nuhu tumejifunza kwamba Nuhu alifanya kwa imani tu yaani kutengeneza safina na kuwaingiza watu wa familiya pamoja na wanyama. Nuhu alimwamini Mungu na lijua kwamba hataweza kuangamizwa, kwasababu alimtii Mungu.
**MB** Rafiki mpendwa, Tukigeuka na kutoka dhambini sasa, na kumuendea Yesu, Yeye atatusamehe dhambi zetu na tutakuwa watu wa familia ya Mungu. Yesu ameahidi kuingia katika mioyo yetu na kuishi milele. Yesu mwenyewe atatupa nguvu na kutusaidia kumpendeza Mungu. Pia Yesu ameahidi kwamba atakapo kuja atatupa mwili mpya, nasi tutafanana naye na tutaishi pamoja na Yesu milele.